Jinsi ya kuweka mwonekano wa Giza YouTube.
Je wajua?
Najua utakua upepitia makala zetu ambapo tulisha fundisha kuhusu kuweka mwonekano wa Giza Google play store na Facebook basi kwa Siku ya Leo tutazungumzia YouTube nia yetu no tujikinge dhidi ya mionzi mikali machoni ndio maana tunatoa mafunzo haya.
Kama unavojua kwamba mwanga mweupe sio rafiki kwa macho na pia kama unavyojua kwamba nayo simu wakati mwingine sio nzuri kwasababu inaweza kukusababishia matatizo ya macho ndio maana tumekuletea makala hii ambayo tutakufunza namna ya kuweka mwonekano wa Giza youtube ili ikusaidie na kukuepusha na matatizo ya macho.
Bila ya kupotenza muda twende tukajifunze moja kwa moja nini cha kufanya ili kuweka mwonekano wa Giza YouTube. Chakwanza kabisa fungua simu yako kisha nenda katika application ya YouTube na mwanzo kabisa pembeni upande wa kulia utaona picture ya profile yako au erufi ya mwanzo ya jina lako bonyeza.
Utaletwa upande mwingine ambapo apa utatakiwa kuchagua setting baada ya kushuka chini kidogo.na bonyeza.
Itakuletea options nyingi wewe utatakiwa kuchagua ya kwanza kabisa iliyo andikwa general na kubonyeza.
Utaletwa mwisho kabisa ambapo apa utatakiwa kuchagua sehemu walio andika dark theme.na kubonyeza on.
Moja kwa moja utaona mwonekano umebadilika na umekua mwonekano wa Giza YouTube.
Ni ivyo tu kwa Siku ya Leo asante kwa kufwatilia makala hii mwanzo had I mwisho ambapo sisi tunakupa makala ambazo zinakufunza kutumia smartphone yako.
0 Comments