Ticker

3/recent/ticker-posts

NJIA 14 HALALI ZA KUPATA PESA MTANDAONI

 NJIA 14 HALALI ZA KUPATA PESA KUPITIA BLOG




Kama bado hujajiunga na group letu la whatsapp Kwa maswali na majibu na mafunzo jiunge sasa HAPA



Je unatafuta njia ya kujipatia pesa kwenye mtandao ambayo siyo ya utapeli? Blog ni njia moja wapo unayoweza kuitumia kujipatia fedha huku ukifanya kile ukipendacho. Katika makala hii nitakushirikisha njia 14 unazoweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia blog yako.

Kumbuka! Hizi si njia za kupata pesa za mteremko haraka haraka kwa usiku mmoja. Kamwe usidanganywe na matangazo ya kuwa utafanywa kuwa tajiri mkubwa siku moja. Mambo hayaendi hivyo.

Awali ya yote utahitaji kuwa na blog yako; pia utahitajika kuwekeza rasilimali ya muda au pesa kiasi fulani ili kuweza kuona matokeo kutokana na blog yako.

1. Kuwa wakala

Unaweza kupata pesa kwenye blog yako kwa njia ya kuwa wakala wa wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mara mtu anunuapo kitu kwa kukifikia kupitia blog yako basi utapata gawio.

Baada ya kuchagua bidhaa ya kuitangaza unaweza kutumia ThirstyAffiliates kutawala matangazo hayo.

2. Jiunge na Google Adsense

Kama una watembeleaji wengi kwenye blog yako kuanzia 1,000 au zaidi kwa siku, unaweza kujiunga na huduma hii na ukapata pesa kutokana na matangazo yatakayowekwa na Google kwenye blog yako.

Aina za utangazaji wa Google Adsense:

CPC – Cost Per Click ni matangazo ambayo utalipwa kadri watumiaji wa blog yako wanavyobofya au kuclick tangazo husika. Kiwango cha malipo kwa click hutegemea kiwango kilichowekwa na mtangazaji.

CPM – Cost Per Thousand impressions ni matangazo ambayo utalipwa kutokana na tangazo kuonwa mara 1,000.

Soma pia: Mambo 9 ya Kuzingatia Wakati Wa Kuchagua Kampuni ya Matangazo Kwenye Blog

3. Njia ya kuweka matangazo moja kwa moja

Unaweza kukubaliana na kampuni husika moja kwa moja kuweka tangazo lao kwenye nafasi fulani ya blog yako. Kwa njia hii unaweza kupata pesa zaidi kuliko kutumia huduma nyingine ambazo ndizo hukubaliana na makampuni husika au mtangazaji.

4. Andika posti iliyodhaminiwa

Hii ni post inayoandikwa kwa lengo la kufafanua au kutangaza huduma au bidhaa fulani. Kampuni husika itakulipa kwa kuandika post inayoelezea na kutangaza bidhaa au huduma yao.



5. Uza blog

Kuuza blog? Ndiyo, kuuza blog kunaweza kukupatia kipato kizuri kabisa. Kama unajua kusanifu na kutengeneza blog, basi unafahamu kitu cha ziada. Kuna watu wengi wanahitaji kununua blog zilizotengenezwa tayari. Unaweza kutafuta anwani nzuri (domain) na kuitengenezea blog kisha ukaiuza kupitia tovuti kama vile Flippa na kujipatia pesa.

6. Tengeneza maudhui ya wanachama

Unaweza ukatengeneza maudhui kwenye blog yako ambayo yanaweza kufikiwa na wanachama waliojisajili tu. Unaweza kupata pesa kwa njia ya kuwatoza ada ya usajili au uwanachama wale wote wanaohitaji kujisajili kwenye blog yako. Kwa njia hii utajipatia kipato moja kwa moja kutokana na wanachama watakaojisajili ili kusoma maudhui hayo.

7. Uza vitabu pepe

Kama una maarifa fulani unaweza kuyaweka kwenye mfumo wa vitabu pepe (e-books) na kuuza vitabu hivyo ili kujipatia pesa. Unaweza ukatengeneza kitabu chako katika mfumo wa PDF na kuwatoza watu kiasi fulani cha pesa ili kuweza kukipakua.


Kama ilivyo kwenye swala la vitabu, unaweza pia ukandaa kozi za kuwafundisha watu mambo mbalimbali unayoyafahamu. Andaa kozi vizuri na kwa ubora, zitangaze kwenye blog yako na watu wanaweza kujiunga kwa kulipa ada fulani ambayo itakupatia pesa.

9. Tafuta kazi kwa kuuza ujuzi wako

Kama una ujuzi wa kufanya kazi au jambo fulani unaweza kutumia blog yako kujitangaza na ukajipatia kipato cha kutosha. Watu wanapotembelea blog yako wanaweza kuvutiwa na ujuzi wako hivyo wakakuajiri ili uwafanyie kazi fulani.



Kama unauwezo wa kuwashauri watu au kuwahamasisha juu ya maswala mbalimbali ya maisha, unaweza kutumia blog yako kufikia wateja wako. Unaweza ukawahudumia kupitia mtandao au ukawaalika moja kwa moja ofisini kwako. Maswala haya yanaweza kuwa tiba, mahusiano, elimu, uchumi, malengo, maono n.k. Unaweza kuwatoza gharama fulani kutokana na huduma husika na ukajipatia pesa. Mfano mzuri wa blog ya namna hii ni blog ya fadhilipaulo.com

Kama unatumia WordPress kwenye blog yako unaweza kutumia WooCommerce plugin kuanzisha duka la kwenye mtandao na ukauza bidhaa mbalimbali. Kwa njia hii unaweza kuuza bidhaa zako au za watu wengine na ukajipatia kiasi kizuri cha pesa.

Soma pia: Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao

12. Uza mavazi yenye chapa yako

Kama unachapa (brand) maarufu ama ya blog au kampuni yako unaweza kuitumia kuuza mavazi na ukajipatia pesa. Unaweza kuuza mavazi yenye chapa yako kama vile tisheti, kofia, mikanda, bangili, mikoba, viatu n.k kupitia blog yako.

13. Uza kazi ya usanifu mtandao

Kama unajua kutengeneza plugins za wordpress, extension za Joomla, violezo (themes/templates) n.k unaweza kuvizua kupitia blog yako na ukajipatia kiwango kizuri cha pesa.

14. Pokea msaada

Hii ni njia ambayo si maarufu sana lakini inaweza kukuwezesha kupata pesa. Umewahi kufikiri tovuti kama wikipedia inajiendeshaje? Inajiendesha kwa kutegemea michango ya misaada ya wasomaji wake. Kama unatoa maarifa au huduma fulani nzuri bila malipo kwanini usiombe msada kwa mtu anayependa kufanya hivyo? Unaweza ukapata kiwango kizuri cha fedha kupitia njia hii.

Hitimisho

Naamini umeweza kufunguka macho na kuona fursa ambazo hukuwa umeziona ua kuzielewa vyema mwanzoni. Ni vyema ukafahamu kuwa hakuna njia ya mkato kupata pesa. Ni vyema ukajitahidi kufanya bidii na kuwekeza muda au fedha kiasi fulani kwenye blog yako ili uweze kujipatia kipato kizuri.

Je una swali au unafahamu njia nyingine bora zaidi ya hizi zilizowekwa hapa? Njoo whatsapp group Kwa discussion



Reactions

Post a Comment

0 Comments